2012-10-04 09:46:21

Vatican yaunda mtandao mpya wa App kwa ajili ya Iphone.


Vatican Radio imetoa mtandao wake mpya wa App, kwa Iphone. Kama ilivyotangazwa wakati wa uzinduzi uliofanyika mapema Septemba 2012, hili ni jukwaa jipya la Android, App katika mfumo wa vyombo vya habari. Una uwezo wa kusikiliza moja kwa moja, katika njia tano, matangazo yote ya idhaa za Radio Vatican, yanayotolewa katika lugha lugha 40 tofauti, ikiwemo kuona video, tovuti za mtandao, taarifa za habari, vyote vikiwa vimeunganisha katika katika chombo hiki moja, kinachoruhusu kufahamu na kufuatilia habari za matukio muhimu ya kila siku ya Papa, na Kanisa kwa ujumla.

Huduma hii ya App, haina malipo, inaweza kupakuliwa kutoka iTunes kwa anwani ya : . Kwa sasa ukurasa umeanza na lugha ya Kiitaliano, Kiingereza, Kifaransa, Kihispania na Kichina). Shukrani kwa mfumo ulioundwa na kuanzishwa na Radio Vatican, "Vatican ICT".
Na taratibu mtandao huu , utaendelea kunasa matangazo katika lugha zingine 39 zinazotoa matangazao yake kupitia Vatican Redio na hasa hotuba za Papa na video za maadhimisho ya Papa, zinazotengenezwa kwa kushirikiana na Kituo cha Televisheni Vatican. Na njia hii , pia itawezesha mtumiaji kuingia katika mitandao ya matangazo ya magazeti zaidi ya sabini katika mipango 40 tofauti lugha ya Radio Vatican. Nyote mwakaribishwa.







All the contents on this site are copyrighted ©.