Jumapili , mtoto mmoja alifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa walipokuwa wamekusanyika
kwa ajili ya Ibada na masomo ya Jumapili, katika Kanisa la Mtakatifu Polycarp, katiak
barabara ya Chai, eneo la Eastleigh, Nairobi Kenya. Maafa hayo yalisababishwa na watu
kadhaa wasiojulikana kutupa bomu katika kanisa la hilo. Polisi Kenya wakithibitisha
tukio hili wanasema, Waliojeruhiwa wengi wao ni watoto waliokuwa wakishiriki katika
masomo ya Jumapili , na walikimbiza ktiak hospitali ya Guru Nanak , baadhi walitibiwa
na kuruhusiwa kurudi nyumbani na wengine kulazwa kutokana na hali zao kuwa mbaya.
Watoto wengine walijeruhiwa kutokana na hali ya kukanyagana baada ya bomu hili kulipuka,
majira ya saa nne na nusu za asubuhi siku ya Jumapili. . Watu watatu mara walitiwa
mbaroni wakati wakijaribu kuchukua picha za tukio hili, ambao wameiambaia polisi kwamba
ni wafanyakazi wa Televisheni ya Somalia. Hali ya mvutano mkali ulijitokeza katika
eneo hilo, baada ya vijana waliokuwa wamekasirishw ana ulipuaji wa bomu hilo, kuanza
kuushambulia msikiti wa Alamin ulio karibu na kanisa lililoshambuliwa lakini polisi
waliweza kutuliza ghasia hizo na kuwataka watu wabaki tulivu. Mwezi Julai , watu
14 waliuawa na wengine 66 kujeruhiwa kufuatia mashambulio mawili pacha katika katika
mjini Garissa Kenya