2012-09-29 16:58:39

Kama watangazaji, mnapaswa kufikisha ujumbe wa Upendo wa Mungu, katika kila miisho yote ya dunia


Kila mwaka tarehe 29 Septemba ambamo Mama Kanisa huadhimisha Siku Kuu ya Malaika Mkuu Gabriel, Radio Vatican pia huisherehekea kama Siku Kuu ya Msimamizi wake Malaika Gabriel.
Kwa ajili ya Siku Kuu hii, Askofu Mkuu Angelo Becciu, Mwenye cheo cha kumkaimu Katibu Mkuu wa Vatican, aliongoza Ibada ya Misa katika kanisa la ndani ya jengo la Radio Vatican, Ibada iliyopambwa kwa sauti nzuri za Waimbaji wa Redio Vatican .
Katika homilia yake , alitaja wafanyakazi wa Redio Vatican kwamba, wana bahati ya kipekee, ya kuwa watu wa kwanza, kufahamu mawazo na nia za Kanisa na hasa mawazo ya Papa na utendaji wake. Wao ni watangazaji wa kwanza wa habari njema za Kanisa , kama ilvyokuwa tangu mwanzo wa kanisa, hadi leo, hitaji la utume huo kupelekwa katikA mipaka yote ya dunia, bado muhimu.
Aliendeela kukumbusha kwamba, kipaumbele cha kwanza katika utume wao ni kufahamisha dunia , mafundisho na miongozo inayotolewa na Papa na Kanisa, ili sauti ya Papa, kupitia kwao , iweze kusikika katika lugha nyingi , hata katika maeneo ya ndani kabisa vijijini , ikijipenyeza na kuishi kupitia vyombo vya redio nyingine , televisheni , magazeti na tovuti za mitandao. Alisema, na itokee kama Malaika Gabriel kwa Maria , kisiri katika nyumba ya Maria ya Nazareth, na alitangaza ujumbe wa Mungu kwa Bikira Maria, ujumbe huo, haukubaki ndani ya nyumba ya Maria lakini ulienea duniani kote, ukipeleka habari njema na tumaini , "Furahini, Furahini , enyi watu wa Mataifa yote".
Askofu Mkuu Bacciu , alieleza na kusema Utume huo wa kutangaza habari njema uliofanywa kwa mara ya kwanza na Malaika Gabriel hadi leo haujabadilika. Ni kazi ya kufikisha ujumbe wa upendo, wokovu na tumaini , lililoletwa na Kristu duniani, ikionyesha kwamba, Mungu aliupenda ulimwengu huu hata akamtoa Mwana wake Pekee, ndivyo anavyotupenda sote.
Kwa hakika ninyi ni wasaidizi, katika kazi za kitume za Kiongozi wa kanisa la Ulimwengu, Khalifa wa Mtume Petro na decania yote kitume, katika agizo, nendeni dunianikote mkatangaze habari njema kwa kila kiumbe. Ninyi pia katiak huduma ya Khalifa wa Mutme Petro na Mitume, mko pamoja nao mkiwa kati ya waliotumwa kwenda kuhubiri iwe katika hali za kimyakimya na kwa ukarimu, mkiwa nyuma ya maneno ya Papa, , kama vyombo vya utangazaji wa habari njema na furaha kuu kama ilivyokuwa kwa Malaika Gabrieli.
Pia aliongeza kwamba kwa kazi yenu, pia mnatakiwa kusimama imara katika kutangaza habari hii njema ya wokovu wa Kristu , hata katika mazingira magumu yanayoonekana kuwa hatarishi. Ni muhimu kutoa pia habari zinaoonyesha maovu dunaini, ili watu wapate kutambua yaliyo mema na maovu. Bila shaka hata Maria aliishi kipindi hiki cha uchungu wakati habari za kifo cha mwanae Golgota zikienea.
Na kwenu kama ilivyokuwa kwa kila mpelekeaji wa habari kwa jamii anaweza kukumbana na ukatili wa kibinadamu , lakini dumuni ktiak imani kama ilivyokuwa kwa Maria , sote tumealikwa kuamini habari njema ya wakati wa mapambazuko ,ya ufufuko wa Bwana.
Na mwisho, kwa niaba ya Papa alionyesha furaha yake na shukurani kwa Wafanyakazi wote wa Redio Vatican kwa kazi na ushirikiano wao , katika kuufikisha ujumbe wa Kristu katika mipaka yote ya dunia .








All the contents on this site are copyrighted ©.