2012-09-27 15:03:04

Tahariri- Haki ya Kimataifa


Mahakama ya Kimataifa mjini The Hague, hivi karibuni ilitoa hukumu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa Bwana vita, Thomas Lubanga, wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Na nchini Sierra Leone, Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Sierra Leone, iliyosikiliza kesi ya Rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor, alimhukumu miaka 50 jela. Katika kesi zote mbili , sehemu kubwa ya maoni ya umma wa Afrika, yalioonyesha kutoridhika na hukumu hizo.

Kwa Thomas Lubanga, Waafrika wengi wanaona adhabu aliyopewa ni nyepesi kulinganisha na uzito wa makosa aliyotenda. Na kwa Charles Taylor, wengi hawakukubaliana na uamuzi wake wa kukata rufaa dhidi ya hukumu. Kesi zote mbili zinaonyesha , ni kiasi gani Afrika inajitahidi kuifanya dunia iieleweke katika masuala haya ya haki. Na tukiongeza katika wazo la wale wanaoamini kwamba , haki haitaweza kutendeka hadi hapo utendaji wa haki ufanyike dhidi ya uhalifu wa wote, na si kwa ajili ya Afrika, hali itabaki katika mkanganyiko wa jumla.

Ni kweli kwamba leo dunia iko katika mageuzi nyeti na wakati mwingine bila hoja kimantiki. Wahalifu wanaweza kujulikana lakini wale wanaowatuma kufanya hivyo wanabaki kuwa watu huru, pamoja na nia na mifumo iliyo nyuma na uhalifu msingi ya uhalifu huo kuwa mambo yasiyo gusika. Mbali na hilo, haki inabaki kuwa mchakato mgumu. Haikomi kutokana na hukumu kutangazwa, bali huendelea kutafuta haki kamili, licha ya kiwango fulani cha ukali, unaoweza kufanyika wakati wa kesi kusikilizwa na usawa katika uchaguzi wa adhabu.

Papa Benedict XVI , mara kwa mara amezungumzia suala hili katika mtazamo wa dhamiri kwa kila mmoja wetu. Taratibu za sasa za utandawazi, zinalazimu kushirikishana majukumu. Hali hiyo inahitaji viongozi kutuongoza kwa mujibu wa sheria, kutenda kwa namna za kutopandikiza ukosefu wa haki. "Vile vile, katika muktadha usio kuwa na umuhimu au sababu za maendeleo duni ya kitamaduni, tunapata shida za mifumo hiyo kujirudia rudia. Papa Benedict XVI, ameandika katika waraka wake wa Upendo katika Ukweli “ Caritas in Veritate (No.22).

Katika matukio yote mawili ya Sinodi Maalu m za Maaskofu kwa ajili ya Bara la Afrika, Sinodi ya 1994 na ile ya mwaka 2009, Maaskofu wa Afrika walisisitiza masuala ya amani Haki, na maridhiano, na kama ilivyo aswa katika Waraka wa Dhamana ya Afrika “ Africae munus”, Benedict XVI anakumbusha kwamba, mchakato wa amani na maridhiano, una wawajibisha wahalifu na kafara na pia mamlaka husika.
anayetenda wakosaji na waathirika kama vile mamlaka. "Kama ni kuwa na ufanisi, maridhiano hyana lazima yaambatane na utendaji wa kijasiri na uaminifu : kuwajibisha wote wale waliohusika na migogoro hii, wale wanaojihusisha na mifumo hii ya uhalibifu wa kial aina na nia zao . Waathirika wana haki katika kweli na haki. Ni muhimu kwa sasa na ya baadaye ya kusafisha kumbukumbu, ili kujenga jamii bora ambapo majanga kama hayo hayarudiwi tena "(Africae Munus, No 21).

Wito wa Kanisa inaonyesha hatua ya kuanzia na kutoa mwelekeo wa kufuata: Haki ya watu, wakati inaonekana katika mchoko iweze kuchota nguvu na msukumo katika haki ya Mungu, ambayo inatoa "upeo wa macho ambayo ni lazima huwa kama ni kuwa mkamilifu, "(Africae Munus, No 25). Na kuwa upeo kutoka kwa Mungu Mkamilifu, ambaye ni upendo, haki tu inayoweza kuongoza katika misingi, isiyopandikiza hasira, kukanganyikiwa au chuki. Na iwezekane kwa viongozi kueleweka , na Iwezekane kwa watu na hasa wabatizwa, kuishi katika maisha yao ya kila siku.

Imeandikwa na Albert Mianzoukouta, Idhaa ya Kifaransa Afrika, Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.