Wakristu Nigeria , hawaogopeshwi na mashambulio ya kighaidi Makanisani- asema Mhashamu
Askofu Mkuu Ignatius Kaigama.
“Ukweli ni masikitiko makubwa pamoja na kuwa kulikuwepo na ulinzi lakini walipata
namna ya kuweza kuwashambulia na kulipua waamin waliokuwa wakisali jumapili iliyopita”,
hayo yalisemwa na Askofu Mkuu Ignatius Ayau Kaigama Rais wa Baraza la Maaskofu nchini
Nigeria, wakati akizungumza na shirika la habari la Fides, juu ya bomu lilipuliwa
jumapili katika kanisa kuu katoliki la Buachi kaskazini mwa Nigeria. Bomu hilo lililipuliwa
na mmoja wanaharakati wa kiislamu wasiovumilia wengine , kikundi cha kigaidi cha
Boko haram.
Askofu Mkuu Kaigama, ameyaita mashambulio haya kuwa ya kusikitisha
maana mtu huwezi kuwa na uhakika wako wapi, na kwa nini wanafanya hivyo, maana wakati
wote wanaweza kujitokeza. Alisema hayo akiwa anaelekea kuwaona waamini wake na hakuwa
na uhakika kama atarudi nyumbani kwa sababu watu wakatili wa namna hii wanaweza kufanya
chochote kibaya lakini hata hivyo alisema kuwa inabidi kuendelea mbele katika maisha
yao na shughuli zao za kila siku bila kuogopeshwa na ugaidi huo.
Mashambulizi
mengine yalitokea huko katikati ya wiki iliyopita aliyekufa ni kijana na mwanamke
mmoja pamoja na huyo mtu aliyelipua hilo bomu kwa makusudi akiwa ameweka bomu ndani
ya gari lake lililokuwa limeegeshwa karibu na mlango wa ulinzi nje kidogo ya kanisa
kuu.
Kuhusiana na mashambulizi hayo ya kigaidi Askofu Mkuu Kaigama anaeleza
kuwa kundi la kiislam la Boko haram, lililoibuka tangu mwaka 2010 limeshaua watu 1,400
katika mashambulizi yaek sehemu mbalimbali, kanisani, ofisi za serikalini na katika
majumba ya ulinzi au masoko.