2012-09-26 15:44:21

Papa ataja umuhimu wa kushiriki Ibada za Kiliturujia katika maisha ya muumini


Baba Mtakatifu Benedikto XV1, akitoa Katekesi kwa mahujaji na wageni, mjini Vatican, baada ya kuitafakari sala ya muumini kwa muda wa wiki kadhaa , kulingana na mafundisho ya Maandiko Matakatifu, wiki hii aligeukia kipengere kingine muhimu na nyeti katika Sala nacho ni liturujia .
Alianza kutoa ufafanua wa neno"Liturujia "akisema, katika asili ya lugha ya Kigriki, lina maana ya "kazi inayofanywa na watu kwa ajili ya watu. Na watu hao wanaotajwa ni watu wa taifa jipya la Mungu, lililoundwa kupitia Kristu , taifa lisiloweza kuwepo lenyewe, isipokuwa kwa kufungamanishwa na damu ya Kristu, nchi inayoundwa kupitia njia ya Fumbo la Pasaka. Liturujia ni pia "kazi ya Mungu". RealAudioMP3








All the contents on this site are copyrighted ©.