Papa kuwa na ratiba nzito Octoba na Novemba- Vatican
Baba Mtakatifu Bendikto XV1, kwa mwezi Octoba na Novemba, ana ratiba nzito, kama
ilivyotajwa na Ofisiya Liturujia za Kipapa. Shughuli zimeongezwa na uwepo wa Mkutano
13 wa Sinodi ya Kawaida ya Maaskofu, kufunguliwa kwa mwaka wa imani, na ibada ya kutaja
Watakatifu Wapya. Mkuu wa liturujia za Kipapa, Mons. Guido Marino, ameeleza wakati
akitoa ratiba ya liturujia zitakazoongozwa na Papa katika kipindi cha mwezi Octoba
na Novemba 2012, akisema, Ibada za Misa na sala za kuombea sinodi zitakazo tolewa,
ni matukio muhimu, ni wakati wa neema na mwanga wa Kanisa. Papa anaianza ratiba
hapo Alhamis 4 Octoba, atakapo tembelea Madhabahu ya Loreto ambako anakwenda kupiga
magoti mbele ya Madhabahu ya Mama Bikira Maria kuomba msaada wake kwa ajili ya baraka
za mwaka wa Imani. Tarehe 7, ambayo ni Jumapili ya XXV11,majira ya saa tatu na
nuzu za asubuhi ataongoza Ibada Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya
kufungua Sinodi ya Kawaida ya Maaskofu ya 13, ambamo pia atawatangaza rasmi kuwa walimu
wa Kanisa, Mtakatifu Yohane wa Avilla na Mtaktifu Ildegarda wa Bingen. Alhamis
11 Octoba, Papa ataongoza Ibada ya Misa katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
majira ya saa nne za asubuhi, kwa nia ya kuufungua mwaka wa imani. Na tarehe 21
Octoba ambayo ni Jumapili ya XXIX ya mwaka, Papa ataongoza Ibada ya Misa katika uwanja
wa Kanisa Kuu la Mtaktifu Petro majira ya saa tatu na nusu , kwa nia ya kuwataja kuwa
Watakatifu, Wenye heri wafuatao: - Giacomo Berthieu- Pedro Calungsod,- Giovanni Battista
Piamarta,- Maria del Monte Carmelo Sallés y Barangueras,- Marianna Cope.- Caterina
Tekakwitha Anna Schäffer. Tarehe 28 Octoba, ambayo ni Jumapili XXX, Papa ataongoza
Ibada ya Misa katika Altare ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa nia ya kufunga Sinodi
ya Maaskofu ya 13. Na tarehe 2 Novemba, Papa atatolea sala zake akiwa katika
mapango ya Vatican ambako atawakumbuka Marehemu wote na Mapapa Marehemu . Jumamosi
tarehe 3 Novemba , saa tano na nusu, Papa ataongoza Ibada ya Misa katika Altare ya
Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa nia ya kuwaombea Makardinali, Maaskofu Wakuu na
Maaskofu, waliofariki ktika kipindi hiki cha mwaka mmoja.