2012-09-20 08:59:29

Papa ataja majina ya Wajumbe wa Sinodi ijayo.


Baba Mtakatifu Benedikto XV1, Jumanne alitaja majina ya wajumbe maalum 36 watakaoshiriki katika Sinodi ya Maaskofu ya Kawaida , itakayofanyika hapa Vatican kwa muda wa wiki tatu -7-28 Octoba 2012. Licha ya wajumbe walioteuliwa na Papa, pia kila Baraza la Maaskofu Katoliki Kitaifa, litatuma mjumbe wake.

Sinodi hii itatafakari kwa kina juu ya mada: Uinjilishaji Mpya, kwa ajili ya kueneza Imani ya Kikristu.

Toka Afrika wajumbe walioteuliwa na Papa siku ya Jumanne ni , Muadhama Kardinal Polycarp Pengo wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam, Tanzania, mwingine ni Mhasamu Askofu Mkuu John Onaiyekan wa Jimbo Kuu la Abuja, Nigeria na Askofu Menghsteab Tesfamariam wa Jimbo la Asmara in Eritrea.

Papa Mwezi June, alitaja majina matatu ya watakao kuwa Marais wa Sinod, nao ni Muadhama Kardinal John Tong Hon, wa Jimbo la Hong Kong, pia Muadhama Kardinali Francisco Robles Ortega , wa Jimbo Kuu la Guadalajara Mexico, Na Muadhama Kardinali Laurent Monswemgo Pasinya wa Jimbo Kuu la Kinshasa DRC.













All the contents on this site are copyrighted ©.