Ni dhambi kubwa kulazimisha muathirika kufunga kizazi
Viongozi wa kidini nchini Kenya wameonya kwamba, huduma za kulazimisha wanawake wanaoishi
na virus vya HIV kufunga kizazi haZikubaliki , maana kufanya hivyo , ni kutenda kinyume
na haki msingi za wanawake. Viongozi wa kidini Kenya wametoa tamko hili kupitia
mtandao kwa ajili ya watu wanaoishi na virus vya HIV na Ukimwi (KENERELA+). Viongozi
hao wameonyesha kujali uwepo wa huduma hii, inayo fanywa kinyume na matakwa ya wanawake
wanaoishi na virus vya HIV, walio bado katiak umri wa kupata watoto. Viongozi
wa Kidini wanasema huduma hiyo si tu iko kinyume na ubinadamu bali pia ni kuwanyanyapaa
waathirika . Na hivyo wote wanaojihusisha na utoaji wa huduma hiyo mbovu, wawajibishwe
kisheria. CISA imetaarifu, Mstaafu Askofu Mkuu Benjamin Nzimbi wa Kanisa la Kianglikan
Kenya , ameonyesha mshangao kwamba, huduma hii ya kufunga kizazi waathirika, inafanyika
wakati huu ambamo sayansi imepiga hatua katika huduma za uzazi . Na hasa katika kuzingatia
kwamba sasa wanawake waathirika wanaweza kujifungua watoto bila ya kuambukiza mtoto
virus. Anasema, juhudi zozote za kumfuga kizazi mwanamke anayeishi na virus kupata
mtoto ni uonevu na dhambi. . Vivyo hivyo Askofu Patrick Mungai wa Kanisa la Kiinjili
Kenya , pia amenukuliwa akilaani huduma ya kuwafunga kizazi waathirika wa virusi vya
HIV, kwamba ni unyama na kinyume cha haki za biandamu, Hoja inayoungwa mkono pia na
Sheikh Abdulllatif Abdulkarim Mratibu wa Maimamu wa Kenya na Ulamaa. Viongozi
wa kidini Kenya wametoa tamko lao kwa kurejea kifungu cha Kikatiba , kinachokataza
mtu kulazimshwa kufungwa kizazi au kuhasiwa kwa nguvu. Kila Mkenya ni haki yake kikatiba
kupata watoto kama wanavyopenda mwenyewe . Na kila Mkenya anayo haki ya kupata huduma
bora za afya ikiwemo huduma za uzazi .