Baba Mtakatifu Benedikto XV1, akikutana na Mahujaji na Wageni, mjini Vatican,kwa nia
za kutoa katekesi kama ilivyo kawaida kwa Jumatano, hotuba yake ililenga katika ziara
yake ya Kimataifa ya 24 ya hivi karibuni, nchini Lebanon. Papa alifanya ziara hii
yakitume tangu Ijumaa 14 -16 Septemba 2012. Ziara inayotajwa kuacha alama kubwa ya
utendaji wa jumuiya dogo ya Kikristu katika jumuiya kubwa ya Waislamu, Mashariki
ya Kati. Jumatano hii, Papa amerudia kutaja madhumuni ya ziara hiyo kwamba ,alikwenda
kutia sahihi na kukabidhi waraka wake wa kitume, alioutoa kama matokeo ya Sinodi
ya Maaskofu, aliyoiitisha maalum Desemba 2010, kwa ajili ya Kanisa Mashariki ya Kati.
Na pia alikwenda Lebanon kwa nia ya kupeleka ujumbe wa amani, kwa watu wa Mashariki
ya Kati , kupitia mikutano na wawakilishi wa makanisa mengine na jumuiya za kikanisa
za Mkoa huo na pia viongozi wa dini ya Kiislamu. Papa aliendelea kuonyesha furaha
toka ndani ya moyo wake kwamba, alifanikiwa kusimama mbele ya watu wateswa wa matukio
ya kusikitisha yanayolemea mkoa wa Mashariki ya kati, na kuhimiza utendaji wenye uvuvio
wa amani katika eneo hilo. Pia Papa amezungumzia kuguswa kwake na imani ya kanisa
mahalia, ambako aliweza kutoa ombi kwa wawaamini kuendelea kukaza nyuso zao kwa Kristu
msulubiwa, mwenye kuwa na uweza wote wa kuwapta nguvu na ushupavu wa kusonga mbele
wakiwa wamejawa na matumaini thabiti katika Kristu , licha ya hali ngumu za majaribu
yanayotaka kudhoofisha juhudi zao za kusherehekea ushindi wa upendo dhidi ya chuki
, ushindi wa msamaha dhidi ya kisasi na ushindi wa umoja dhidi ya migawnyiko. Aidha
Papa kwa mara ingine alionyesha shukurani zake za dhati kwa jumuiya ya Kiislamu, na
hasa kwa makaribisho mazuri na ukarimu mkuu kutoka kwa viongozi wa Kiislamu, wakimezesha
kutoa pendekezo lenye ujumbe wa ujenzi wa majadiliano na ushirikiano miongoni wa jamii
yote ya Lebanon na Mashariki ya Kati kwa ujumla. Mwisho, Papa hakucehelea kuwashukuru
wote walishiriki katika kazi hii ya kufanikisha ziara yake Lebanon. Na kwmba anaendelea
kutoela sala zake kwa mkoa huu mpendwa wa Mashariki ya Kati. Na aliomba msaada wa
Mama Bikira Maria , kufikisha maombi ya watu wa eneo hili, lenye kuwa na madhabahu
nyingi za kale, ili haki na amani vipatikane kwa ajili ya watu wote wa Mashariki
ya Kati.