2012-09-19 15:34:05

kuelekea mwaka wa Imani- Kardinali Stanslaw Rylko


Pamoja na uwepo wa changamoto ngumu, Kanisa bado lina matumaini makubwa katika vyama vya kitume na jumuiya mpya za Wakristu, ambamo mhemko wa imani hulishwa na karama za waumini wenyewe. Katika kuadhimisha mwaka wa Imani , si kama ni tukio la kushereheka, bali ni mwaka wa neema ya Bwana , zawadi inayopaswa kupokelewa kwa moyo wa shukurani na uchaji na uwajibikaji kwa watu wote.
Ni tafakari ya Muadhama Kardinali Stanslaw Rylko, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Walei, kwa wakati huu, tunapo elekea kuuanza mwaka wa Imani , utakaoanza Octoba mwaka 2012. Ameuita ni Kipindi cha kuzama katika “ Safari ya Imani” na kuruhusu kugundua upya kila siku, uzuri wa safari hii ya imani, inayoelekeza katika kumgundua Mungu wa Kweli.
Anasema, " Harakati za kikanisa na jumuiya mpya - pamoja vyama vingine ya walei katika Kanisa leo hii, kweli ni "maabara ya imani"au "shule za imani"kwa kuwa ni , mahali ambamo vijana, watu wazima, wenye ndoa , huweza kutembea pamoja katika njia ya kukutana na Mungu kupitia Yesu Kristu. Na kama anavyoeleza Zygmunt Bauman kwamba , jamii ya leo, ni jamii iliyomezwa na utamaduni wa maonevu, na kuifanya dunia kuwa mahali pasipokuwa na uhakika wa maisha, maisha yasiyokuwa na kumbukumbu wala rejea, isipokuwa kumezwa harara za mambo ya mpito kama fedha, anasa na mali, maisha ya kukanganyikiwa.
Kardianli Rylko anaasa, kwenye hali hizo, harakati za kikanisa na jumuiya mpya kuiimarisha imani yake kwa Kristu , linakuwa ni jambo lisiloweze kukwepeka, kwa ajili ya ujenzi wa ukomavu thabiti katika imani. Na hivyo , bila shaka, nafasi hii ya mwaka wa imani , itakuwa ni wakati wa kila mumini kupima imani yake na kuiimarisha zaidi ili aweze kupambana na changamoto zinazomkabili kama yeye mwenyewe binanafsi na kanisa kwa ujumla.
Hata hivyo Kardinali Stanslaw Rylko anasema, utendaji huu thabiti katika imani ni sehemu ya uhuru kila binadamu, unaomhitaji kukaa macho na mambo yanayoweza kuvuruga imani yake. Hivyo basi Mwaka wa Imani, si kama kipindi cha kushereheka, bali ni mwaka wa neema ya Bwana , zawadi nyeti toka kwa Mungu , inayopaswa kupokelewa kwa moyo wa shukurani, uchachi na hisi za uwajibikaji kwa waamini wote.








All the contents on this site are copyrighted ©.