Uwepo wa Kanisa Mashariki ya kanisa si kama makumbusho ya kihistoria bali ni li hai.
Ni maoni ya Muadhama Kardinali Leonardo Sandri, Mkuu wa shirika kwa ajili ya makanisa
ya Mashariki ya Kati, aliyoyatoa baada ya kukamilika kwa ziara ya Kitume ya Papa Benedikto
XV1, mwishoni mwa wiki 14-16 Septemba 2012. Kardinali Sandri, akijibu maswali
ya wanahabari juu ya ziara hii ya Papa anasema , ilikuwa ni furaha kubwa kwa watu
wa Mashariki ya Kati kuwa karibu na Papa katika siku hizo za kihistoria, ziara iliyowawezesha
dunia kuipata picha ya kundi dogo la waumini, kuendelea kubaki imara, bila kutishika,
ndani ya kundi kubwa la wamini wa imani nyingine. Kardinali Sandri amekiri kwamba,
Kwa hakika Papa Benedikto XV1, ameweza kulionyesha tumaini la Kanisa lisilo dhoofishwa
na hali ngumu wala changamoto za kidunia. Na kwamba bado kuna uwezekano wa kuushuhudia
kwa pamoja, upendo Kristu na kanisa lake kwa kwa watu wote, na kuendelea kutembea
pamoja katika hali hizi ngumu. Katika siku hizi za ziara ya Papa , Papa amewezesha
kuionyesha sura ya Kanisa hai la Wakristu Waotodosi mbele ya kundi kubwa la Waislamu
Mashariki ya kati . Kanisa lililo tayari kuushuhudia Upendo wa Mungu, Kanisa linalojishughulisha
na majiundo ya maisha yenye ukweli na upendo kwa kila mmoja hasa kwa lika la vijana,
kama inavyojionyesha katika uwepo wa shule za Kanisa, ambazo milango yake i wazo kwa
wote. Na akiziungumzia wimbi la Wakristu kuikimbia Mashariki ya kati , Kardinali
Sandri , alirejea himizo lililotolewa na Papa , kuona umuhimu wa kuimarisha mshikamano
na Wakaristu wote , hasa katika ufanikishaji wa mahitaji msingi katika yote mawili,
maisha ya kawaida na maisha ya kiroho kwa watu wa Mashariki , kama hatua ya kupunguza
ukali wa mateso na mahangaiko ya kimwili. Na kwamba, kunahitajika kuwa na majadiliano
ya kina juu liturujia, kati ya makanisa Katoliki na makanisa mengine, kwa ajili ya
ufanikishaji wa muugano thabiti zaidi kwa wafuasi wa Kristu, bila kuathiri utambulisho
wa liturujia kwa kila Kanisa. Na hivyo kuna haja ya Mapatriaki na viongozi wa makanisa
mengine kujadili kwa kina suala hili. Kardinali Sandri ameeeleza na kukiri kwamba
njia hii ni ndefu, lakini ndiyo mwanzo, akiutaja mkutano utakaofanyika Desemba kwa
ajili hiyo.