Papa ahimiza kuujua utambulisho wa Kweli wa Kristu na kutembea nae.
Jumapili hii macho ya Kanisa la Ulimwengu na dunia kwa ujumla yalielekezwa katika
uwanja wa Waterfront, Beirut, ambako Baba Mtakatifu Benedikto XV1, aliogoza Ibada
ya Misa majira ya asubuhi. Na baada ya Ibada alikabidhi rasmi Waraka wake wa Kitume
kama matokeo ya sinodi ya Maaskofu aliyoiitisha maalum Desemba 2010, kwa ajili ya
kutazama hali halisi za maisha Kanisa Mashariki ya Kati. Ibada hii ilihudhuriwa
na maelfu ya watu na ilifanyika katika hali ya utulivu na amani. Katika homili
yake Papa, ametoa shukurani zake za dhati kwa viongozi wote wa Kanisa na serikalina
kwa mkoa wote wa Mashariki ya Kati, kwa ukarimu wote waliomtendea tangu alipowasili
katika taifa hili la Lebanon. Alisema, “Nawasalim Mababa na Maaskofu wa Makanisa
ya Mashariki, mikoa ya jirani, na Makardinali na Maaskofu ambao wamekuja kutoka nchi
nyingine. Nawasalimu nyote kwa upendo mkubwa, Ndugu wapendwa kutoka Lebanon na kutoka
katika mkoa huu mpendwa wa Mashariki ya Kati, kwa ukarimu wenu wa kujiunga na Halifa
wa Petro, kumwadhimisha Yesu Kristo, aliyesulubiwa, kufa na kufufuka. Salamu zangu
pia za heshima zimfikie Rais wa Jamhuri, kwa mamlaka ya Lebanon, na kwa viongozi na
wafuasi wa mila nyingine za kidini ambao waliopendezwa kuwa nasi katika Ibada hii”.
...
Baba Mtakatifu akitafakri masomo ya Jumapili hii, aliyolenga zaidi katika
kumtambua Yesu Kristu ni nani, kama ilivyoandikwa katika Injili ya Marko 8:27- 30,
ambamo Yesu anauliza utambulisho wake wa kweli , wakati akisafiri na wanafuzi wake.
“ Na ninyi je, mwasema mimi ni nani(Mk 08:29”). Papa alisema, Yesu anaulizwa swali
hili muhimu , akijua yatakayo mfika baadaye katika maisha yake. Yeye alikuwa anakwenda
Yerusalemu, mahali ambako tukio la wokovu wetu lilitokea."Watu wanasema mimi ni nani?"
(Mk 08:27). Wanafunzi wake walitoa majibu tofauti tofauti sana: Yohana Mbatizaji,
Eliya, mmoja wa manabii! Amebainisha kwamba, leo hii kama ilivyokuwa wakati wa
Yesu, kuna wengi wanaokutana na Yesu njiani, ambao wanashindwa kumkiri kuwa ndiye
Bwana, na kutoa majibu mengine. Papa anasema, pengine hali hii ya kushindwa kutoa
jibu sahihi , inaweza kuwa msukumo na msaada katika kutafuta njia ya kweli. Ni muhimu
kuitafuta njia ya kutembea pamoja na Yesu na kumjua Yeye ni nani. Ni wale tu
walio tayari kumfuata katika njia yake, kuishi katika ushirika pamoja naye katika
jamii ya wanafunzi wake, wanao weza kulitoa jibu sahihi, la kweli, kujua yeye ni
nani. Hatimaye, Petro, ambaye alikuwa akikaa pamoja na Yesu kwa muda fulani, anatoa
jibu lake: "Wewe ni Kristo" (Mk 08:29). Papa aliendelea kusema, Ni jibu sahihi,
lakini kwa ajili ya kuzuia upotoshwaji wa maana ya Kristu, Masiya aliyetarajiwa,
Yesu aliona haja ya kufafanua zaidi , kwamba, Yeye ndiye Kristu Masiya aliye,taarajiwa
atakaye subiriwa kwa ajili ya kumkomboa binadamu dhidi ya dhambi na mauti. Yesu aliongeza
hili, kwa kuwa, alitambua watu wanaweza kutumia kutoa jibu la haraka haraka , Yeye
ni Kristu, lakini katika mitazamo na matumaini ya uongo ya kidunia. Yesu anatangaza
kwa wanafunzi wake kwamba, imempasa kuteseka na kuuawa na kisha atafufuka. Yesu
anataka kuwaelewesha vyema utambulisho wake wa kweli. Yeye ni mtumishi ambaye anatii
mapenzi ya Baba yake, hata kwa kutoa maisha yake. Hii tayari ilitabiriwa na Nabii
Isaya kama ilivyosomwa katika kusoma kwanza. Yesu hivyo, anaonekana kuwa kinyume na
matarajio ya wengi. Yeye ni masiya anayekubali mateso na kifo na kufufuka. Wakati
wa mateso yake yalipoanza Petro alishtuka na kutaka kutoa jibu la upanga , lakini
Yesu anamkanya naye, anakataa kukubali kuwa Mwalimu wake atateswa na kufa! Yesu anawakanya
wanafunzi wake , ili watambue kwamba mtu yeyote ambaye atakuwa mwanafunzi wake lazima
kuwa mtumishi, na hata kukubali kuyatolewa maisha kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
Kumfuatia Yesu maana yake ni kuchukua msalaba wake na kutembea katika nyayo
zake, njiani gumu ambayo inaongozwa si kwa nguvu ya kidunia au utukufu lakini , ni
hiari na uchaguzi wa mtu katika kuifuta hata katika hali ngumu za kupoteza maisha
.
Pia Papa aliutumia muda huo wa mahubiri, kutoa mwaliko kwa waamini na watu
wote , kuzingatia kwamba, Octoba,11 2012, unaanza mwaka wa Imani. Ni wakati wa
kutafakari kwa kina , nia za kumkiri Yesu Kristu kuwa ndiye Bwana wa Maisha. Ni mwaka
wa kuitafakari njia hii uongofu wa dhati. Ni kuwa na muda wa kuzama katika tafakari
za ndani zaidi, juu ya imani, katika matazamio ya kuwa na uzima wa milele na kukua
katika uaminifu wa Kristo Yesu na Injili yake. Baba Mtakatifu alikamilisha homilia
yake kwa kutolea sala yake maalum kwa Bwana ili mkoa huu mpendwa wa Mashariki ya Kati
uweze kuwa mhudumu wa amani na mapatano kwa watu wote.