Papa awasilisha na kutia sahihi waraka wake wa Kitume kwa ajili ya Mashariki ya Kati
Ijumaa 14 Septemba 2012, Kanisa Mashariki ya Kati, lilishuhudia tukio la Baba Mtakatifu
Benedikto XV1, kuwasilisha na kutia sahihi waraka wake wa kitume kwa ajili ya Mashariki
ya Kati. Uwasilishaji huo ulifanyika mbele ya viongozi mbalimbali wa Kikanisa, Mapatriaki
na Maaskofu, na pia viongozi wa kisiasa akiwepo Rais wa Lebanon, Michel Sleiman, pia
Rais wa Bunge la Lebanon , Mheshimiwa Nabihi Berri na Rais wa Baraza la Mawaziri,
Wajumbe wa Baraza Maalum la Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Mashariki ya kati , na
wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali za kidini, kitamaduni na kijamii . Katika
hotuba yake, Papa amewashukuru wote kwa dhati kwa makaribisho mazuri aliyoyapokea
katiak mkutano huu uliofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo , nakwa pia kwa
wajubme wa Baraza Maalum la Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Mashariki ya kati, na
uwepo wa wawakilishi kutoka Kanisa la Kiotodosi , Waislamu na Wadruze na pia kutoka
jumuiya za kitamaduni na kijamii. Alisema uwepo wao wote unampa idhini ya kutia sahihi
katika waraka huu wenye azimio la Kitume kwa ajili ya Kanisa Mashariki ya Kati, ikishuhudiwa
kwamba , waraka huu pamoja na kulengwa katika Kanisa la Ulimwengu, una umuhimu wa
kipekee katika Mashariki ya Kati yote. Baada ya salaam na Shukurani, Papa alionyesha
pia kufurahia kwamba tukio hili la kukabidhi waraka huo, linafanyika katika tarehe
hii, ambayo kila mwaka Mama Kanisa, huadhimisha siku kuu ya Kutukuka kwa Msalaba
Mtakatifu, Siku Kuu iliyoanza Mashariki tangu miaka ya 335, kufuatia heshima kwa Kanisa
Kuu la Ufufuko lililojengwa katika kilima cha Golgota na Kaburi la Bwana wetu Yesu
Kristu, ujenzi uliofanyika wakati wa Mfalme Constatine Mkuu, Mtakatifu anayeheshimwa
sana Mashariki ya kati . Papa akiwasilisha waraka huu, alihimiza usomwe katika
mwanga wa Siku Kuu hii ya kutukuka kwa Msalaba, ulio jitokeza kwa Constatino wa Chi-
Rho, uliong’ara katika usiku wa kiza , ukiandamana na maneno, "katika Ishara hii ya
Msalaba Utapata Ushindi." Papa amesema, kuna kiungo kisichoweza kutenganishwa
kati ya Msalaba na Ufufuko wa Bwana ambao Wakristu hawawezi kukisahau kamwe. Msalaba
Mtukufu ni kiungo kinacho tuunganisha na Mungu. Bila kuwa na kiungo hiki cha Msalaba
Mtukufu, inamaanisha mateso na kifo ,vinafanya hatima ya maisha ya mtu, kukosa thamani
. Papa aliasa, hivyo kwa Wakristu, Msalaba Mtukufu, ni alama ya muungano kamilifu
na Upendo a Mungu usiokuwa na masharti kwa binadamu. Msalaba Mtukufu ni kitendo cha
imani, kinachomweka muumini karibu na Mungu. Kutukuza Msalaba, ni katika kuwa na
hamu ya kuishi na kuuonyesha upendo huu kailimifu kwa wote. Ni kitendo cha upendo.
Na hivyo kuutukuza Msalaba ni aaniha uwajibika katika utendaji wote wa kila siku,
utendaji wa kidugu na umoja wa kikanisa. Ni chimbuko la ushuhuda wa kweli wa Mkristu.
Na Ni ujenzi wa matumaini.
Papa aliendelea kuitazama hali halisi ya Kanisa
Mashariki ya Kati akieleza jinsi Mababa wa Sinodi walivyoziishi hali hali za Kanisa
katika eneo hili la Mashariki ya kati , furaha na mahangaiko yake , hali za wasiwasi
na mashaka, woga na tumaini la wafuasi wa Kristu katika mataifa ya Mashariki ya kati.
Kwa namna hiyo, Kanisa lilieweza kusikiliza kilio cha hali hizo kutoka nyuso za watu
hawa wake kwa waume wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi katika yote, kimwili
na hata kihali wanaoishi katika hali ngumu za mivutano yenye nguvu katika woga na
ukosefu wa uhakika , kwa wale wanaotamani kumfuata Kristu , mwenye kutoa maana kamili
ya uwepo wao duniani, ambao kw amara nyingi huzuiwa kufanya hivyo na binadamu wengine.
Papa alitoa maelezo hayo na kuendelea kuwaangalisha katika nyaraka mbalimbali
za mitume za Agano jipya , ambazo zinahimiza watu kumtukuza Yule menye kuwa na funguo
zote za maisha , Yesu Kristu, Mwana w Mungu aliyemwilishwa na kukaan a binadamu ili
aweze kumkomboa na kumpa uzima wa Milele. Papa amehoji kwa neema hizi kwa vipi binadamu
ashindwe kumtukuza na kumshukuru kwa ajili ya juhudi zao za kulijenga Kanisa lake
na udugu katika usharika na kwa ajili ya mshikamano wa kibinadamu unaopaswa daima
kuonekana, kwa wote wanaoitwa wana wa Mungu?
Papa amesema, katika mwanga
wa matumaini, Kanisa Mashariki ya Kati huwezesha kufikiri tena juu ya tumaini la baadaye
kwa mtazamo wa macho ya Kristu . Papa akiugeukia waraka aliouwasilisha alieleza
kwamba, Kwa mtazamo wake wa kibilia na kichungaji ni mwaliko wa kuzamisha tafakari
za kiroho na kikanisa , katika wito wake kiliturujia na katika mtazamo wake wa kuhuisha
upya katekesi na agizo lake katika majadiliano, waraka unaonyesha njia kwa ajili
ya kugundua upya jambo msingi katika kuwa wafuasi wa Kristu, hata katika mazingira
magumu na wakati mwingie kwenye hali za kuumiza ambazo hutoa kishwawishi cha kutaka
kupuuza au kusahau kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu. Na ni hapo ambapo waamini wanaitwa
kusherehekea ushindi huu wa upendo dhidi ya chuki , msamaha dhidi ya kulipiza visasi
, huduma dhdi ya ubinafsi, unyenyekevu dhidi ya majivuno, umoja dhidi ya migawanyiko
na utengano. Katika mwanga wa siku kuu hii ya Kutukuka kwa Msalaba, na Katika
mtazamo wa azimo la mwisho la Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Mashariki ya Kati, Papa
amehimza wote kutoogopa , kusimama imara katika ukweli na katika utakatifu wa imani,
kwamba hiyo ndiyo Lugha ya Msalaba Mtukufu. Msalaba wenye uwezo wa kubadilisha hali
ngumu na mashaka na kuwa upendo na matumaini kwa Mungu na jirani.