Baba Mtakatifu aianza ziara ya kitume ya kimataifa ya 24 Lebanon
Kunako majira ya saa tatu za asubuhi Ijumaa hii, Baba Mtakatifu Benedikto XV1, aliianza
ziara yake ya kitume ya kimataifa ya 24 nchini Lebanon, ambako atakuwa hadi Jumapili
16 Septemba 2012. Papa aliwasili katika uwanja wa Rafik Beirut majira ya saa sita
na nusu za adhuhuri kwa saa za Lebanon. Madhumuni ya ziara, ni kama mhujaji wa
Kanisa na Mashariki ya kati yote, anayepeka ujumbe wa amani, wakati anapokutana na
watu mbalimbali, viongozi wa kijamii, viongozi wa kidini na vijana pia. Pia yuko
Lebanon kwa lengo la kuwasilisha na kutia sahihi katika waraka wake wa Kipapa, wenye
tamko la mwisho la kitume, anao uutoa kama matunda ya sinodi Maaskofu aliyoiitisha,
maalum kwa ajili ya Kanisa Masahriki ya Kanisa, Sinodi ya Desemba 2009. Sinodi hii
ilitazama na kutafakari kwa kina hali za maisha ya Wakristu katika mataifa ya Mashariki
ya Kati. Waraka alioutia sahihi na kuuwasilisha hivyo ni majumuisho ya maoni ya
sinodi hiyo kwa Kanisa la Mashariki ya Kati , na utatumika kama mwongozo kwa Kanisa
la Mashariki. Katika siku hii ya kwanza ya ziara, Papa amekuwa na matukio mawili
makubwa katiak ratiba yake , kwanza ni Mapokeziyaliyofanyika katika uwanja wa ndege
wa Rafik wa Beirut nyakati za adhuhuri, na jioni majira ya saa kumi na mbili saa za
Lebanon alitia sahihi na kuwasilisha waraka huo kwa viongozi wa kanisa Mashariki ya
kati. -------