2012-09-12 14:13:14

Ziara ya Papa Lebanon, tumaini katika ujenzi wa amani haki na mapatano Mashariki ya Kati


Ziara ya Papa nchini Lebanon, inatazamiwa kuwa hatua ya kwanza thabiti katika mageuzi ya kujenga amani, haki na mapatano kwa mataifa ya Mashariki ya Kati. Ni tamko kutoka Baraza Kuu la Upatriaki Katoliki wa Armenia, baada ya kikao chake cha jumatano, kilichoongozwa na MwenyeHeri, Nerses Bedros XIX Tarmuni. Kikao kilichofanya mapitio kwa mara ingine, juu ya ziara ya Papa Benedikto XV1, nchini Lebanon, katikati ya mwezi ujao 14-16 Septemba 2012.
Washiriki wa kikao hicho, walionyesha tumaini lao kwamba ziara hii , inayofanyika wakati wa kipeo kikali cha kisiasa katika mataifa mengi ya Mashariki ya Kati, itakuwa kichocheo cha utendaji wa amani, haki na mapatano , kwa watu wote wa Mashariki ya kati.
Baraza limehimiza waamini kutolea sala zao kwa nia ya kumwombea Papa na wote watakao andamana nae katika ziara ya kitume. Pia wameitaka jumuiya ya Katoliki ya Armenia kushiriki kwa wingi katika mihadhara itakayo hutubiwa na Papa , hasa Ibada ya Misa atayo iongoza Jumapili 16 Septemba, katika kituo cha Watefront mjini Beirut.
Na pia wamesisitiza umuhimu wa kutazama kwa makini changamoto zilizotajwa katika Hati ya mwisho ya Kichungaji, juu ya Kanisa Mashariki ya Kati, kama msaada wa kuwasindikiza katika utendaji unaofaa katika hija yao ya kiroho. Ujio huu ni matumaini ya kupata mahali pa kuanzia ujenzi wa amani , mapatano na mshikamano wa kitaifa, si kwa wakristu tu lakini pia kwa Waislamu na dini zingine mahalia.
Mwenye Heri Patriaki Fouad Twal wa Jerusalem , hivi karibuni akizungumza na Redio Vatican, pia alionyesha tumaini lake kwamba ,ujio wa Papa utaweza kuliimarisha zaidi Kanisa, Mashariki ya kati. Na wakati huohuo, alionyesha kufadhaika kwamba, mpaka sasa hakuna hatua madhubuti , zinazoonekana kufanikishaji majadiliano kati ya dini na hasa na Wayahudi, ingawa kuna dalili za nia njema.
Na akitazama mivutano ya kisiasa katika taifa la Syria, ameweka matumaini yake kwa ziara ya Papa, kwamba, itaongeza kishindo katika mbinu za jumuiya ya kimataifa, kufanikisha amani , haki na mapatano katika mkoa wa Mashariki ya Kati.
Papa Benedikto XV1, anafanya ziara hii Lebano kwa mwaliko wa Rais wa Lebanon,Michael Suleiman, na pia anakwenda kuwasilisha maoni yake ya mwisho, juu ya Utendaji wa Kanisa katika eneo la Mashariki ya Kati, kama ilivyoainishwa na Sinodi ya Maalum ya Maaskofu kwa kanisa la Mashariki ya Kati.








All the contents on this site are copyrighted ©.