Madhulumu dhidi ya Wakristu yanaendelea kusikika Pakistan, licha ya viongozi mbalimbali
wa kimataifa kukemea dhuluma hizo. Fides imeripiti kwamba, Augosti 14,
binti wa miaka 15 , alibakwa na kundi la wanaume watano na kuuawa kikatili karibu
na mji wa Sahiwal Punjab. Ni tukio jingine lililoumiza roho za Wakristu, ambalo taarifa
zake zililifikia shirika la habari la Fides , wakati Mahakama ikisikiliza kesi nyingine
ya madhulumu ambamo mtoto Mkristu wa miaka 11 , mwenye udumuavu wa akili , kukamatwa
na ameikashfu korani . Habari inasema, kijana huyo Rimsha Masih , ambaye
huwa na tabia cha kuchakura mapipani kutokana akili yake duni inavyomtuma, aliokota
karatasi hizo za koran pipani. Watetezi wake wanasema, ni ukosefu wa ubiandamu
kumweka jela Rimsha, ambaye hata hajui kusoma wala kuandika. Hivyo karatasi hizo
za koran alizokutwa nazo, kwake yeye Rimsha zinaokena hazina tofauti na vitu vingine
alivyookota mapipani. Kesi hii imevutia wengi , kutaka kujua hatima ya
kijana huyo.