2012-09-12 14:12:56

Wakatoliki Nigeria, hawatatoa jibu la upanga kwa upanga.


Wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa wa Utendaji Katoliki( IFCA) uliofanyika Iasi Romania , tangu tarehe 22 hadi 26 Augost , wameoneysha kujali kwamba, Wakatoliki katika mataifa mengi ya Afrika, wanaishi na hali za vitisho kutoka kwa Waislamu wenye siasa kali. Lakini huziishi hali hizo bila kudhamiria ulipizaji wa kisasi au kujiingiza katika ghasia.
Padre Patrick Alumuku, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano jimboni Abuja Nigeria, akishirki mkutano wa IFCA, alieleza jinsi Wakatoliki Nigeria hawatishiki na mashambulio yanayofanywa na wababe wa kiislamu katika makanisa .
Na ametaja juhudi zinazofanyika sasa kulinda maeneo ya ibada na makanisa, kwamba, kwa kushirikiana na Polisi , Wakristu , wameunda vikundi vya ulinzi katiak maeneo yao na maeneo ya ibada na makanisa, kama nji apekee yenye uhakika wa kutoshambuliwa na waovu. N
Hilo limefanyika kuitikia wito wa viongozi wa kanisa akiwemo Askofu Mkuu John Olorunfemi Onaiyekan wa Jimbo la Abuja, unao wataka Wakristu wasitoe jibu la jino kwa jino, kwani jibu kama hilo hilo haliwezi kutatua matatizo, bali kuleta uhasama zaidi.
Na kwamba Wakristu wanaelewa, uislamu haushambulii Ukristu, lakini mashambulio hayo, ya kighaidi yanafanywa na watu wachache wenye uchu wa madaraka , wanaotaka kuiagusha serikali iliyopo kupitia mgogo wa dini. Kwa Wakristu jaribio lolote la kutaka kulipiza kisasi , ni kutenda kinyume cha Injili" Heri walio wapole maana wataurithi Ufalme wa Mbinguni".
Na Padre Rafik Greiche, Msemaji wa Kanisa Katoliki Misri, pia alieleza hali ya vitisho wanayoishi nayo Wakaristu nchni Misri hasa baada ya mabadiliko ya utawala. Pamoja na Rais mpya wa Misri, kutoa ahadi za kutetea makundi madogomadogo ya kidini hakuna anayeweza kuwa na uhakika kwa siku za baadaye. Katika hali hiyo, shuhuda za Kiinjili za walei zinabaki kuwa jambo muhimu sana katika maisha yao ya kila siku na katika kupambana na changamoto mbalimbali , kwa ushupavu na hekima nyingi.








All the contents on this site are copyrighted ©.