Wazo Kuu katika Tahariri ya Wiki hii ya Padre Federico Lombardi, Mkurugezi wa
Radio Vatican, ni ”Kuelekea Lebanon”. Padre Lombardi, anasema, wengi wanaitaja
ziara hii kwamba inaonyesha Ushupavu na matumaini makubwa ya Baba Mtakatifu Benedkito
XV1, katika ufanikishaji wa umoja na amani, katika kila kona ya dunia.
Papa anakwenda Lebanon , kuwasilisha waraka muhimu wa maisha na utume wa Kansia Katoliki
katika eneo la Mashariki ya Kati,katika kuishuhudia Injili ya Upendo wa Kristu na
uwajibikaji wa Kanisa kama chombo cha kuhamasisha majadiliano na amani miongoni mwa
jamiiya Mashariki ya Kati. Lebanon, ambayo ina idadi kubwa ya Wakatoliki,
ilichanguliwa tangu mapema, hata kabla Syria haijaingia katika machafuko ya kisiasa,
yenye umwagajiwa damu yanayoendelea sasa.