Baba Mtakatifu Benedikto XV1, amehiza utamadunishaji sahihi wa Imani, ili Injili
iwe sehemu ya utamaduni wa watu mahalia, kuishi upendo wa Kiinjili , upendo kwa jirani.
Msisitizo huo aliutoa Ijumaa iliyopita, 7 Septemba2012 , aliwahutubia Maaskofu wapya
wapatao mia, waliokusanyika katika ukumbi wa Swiss Hall, uliopo, makazi ya Kipapa
huko Castel Gandolfo. Maaskofu wapya wamekusanyika Roma kwa lengo la kuhudhuria
kozi ya majiundo ambayo hutolewa kwa Maaskofu wapya wateule,kama inavyoandaliwa na
Shirika la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji wa Watu. Papa katika hotuba
yake kwa maaskofu wapya, alisifu kukua kwa Kanisa barani Afrika Asia, Amerika n a
Oceania , akisema, kushirikishana furaha hai na ubunifu katika imani, hasa unaofanywa
na Jumuiya za Vijana Katoliki, ni ishara ya tumaini kwa ajili ya mustakhabli wa Kanisa
la Ulimwengu