Mlei ashuhudia umuhimu wa Kongamano la Walei linaloendelea Yaounde Cameroon
Kongamano la Kimataifa la Walei Wakatoliki , linalo hudhuriwa na washiriki kutoka
toka pande mbalimbali za Afrika, Wakatoliki walei na viongozi wao, Maaskofu na Mapadre
na watawa pia , linaendelea huko Yaounde Cameroon, kama ilivyoandaliwa na Baraza
la Kipapa kwa ajili ya Walei. Padre Moses Hamugole, Mkuu wa Idhaa ya Kiingereza
na Kiswahili Radio Vatican, akishiriki katika kongamano hili, alipata nafasi ya kumhoji
Queen Said, Mlei toka Tanzania na Mwana jumuiya ya Mtakatifu Egidio, na anatumegea
hisia zake kwamba: Kongamano
hili la siku tano , 4-9 Septemba 2012, lilifunguliwa Jumanne kwa Ibada ya Misa, mjini
Yaounde Cameroon , na linaongozwa na Mada ” Mashahidi wa Yesu Kristu Afrika leo hii.
Ninyi ni Chumvi ya Dunia na Mwanga wa Ulimwengu, lengo lake ni kushirikishana uzoefu
wa maisha leo hii katika kuieneja Injili ya Upendo wa Kristu kwa watu wote. Mkutano
pamoja na kushirikishana uzoefuwa maisha na maoni yanatazamishwa zaidi katika waraka
wa dhamana kwa Afrika, uliotiwa sahihi na Papa Benedikto XV1 na kuukabidhi kwa Kanisa
barani Afrika, kama mwongozo wa kutembea pamoja kiliturujia na kichungaji katika
neema za hija ya kanisa barani Afrika. Papa anasema, huu ni wito kwa kila muumini
mbatizwa kuwa chumvi ya dunia na mwanga wa ulimwengu. . Papa amelitaja
kongamano hili Walei linaloendelea Cameroon kuwa na umuhimu wake katika kupata mang’amuzi
ya uvuvio wa Roho Mtakatifu kwa Mababa wa Sinodi ya Pili ya Maaskofu, iliyoandaliwa
Maalum kwa Kanisa la Afrika , Sinodi iliyofanyika Octoba 2009 hapa Roma.
Kwa ajili hiyo, Papa ameonyesha furaha yake, kwa uwepo wa Kongamano hilo la Walei
ambamo Walei wanaitwa kwa namna ya pekee kulitumika Kanisa Shamba la Bwana, katika
nyakati zetu. Kama pia alivyoeleza Papa Yohane Paulo 11, katika waraka wake wa Kanisa
barani Afrika, alioutoa kama matokeo ya sinodi ya kwanza ya Maaskofu iliyoandaliwa
maalum kwa Kanisa barani Afrika, Octoba 1994. . Papa Benedikto XV1, kwa
mara ingine amerudia tena kulitaja bara la Afrika kuwa ni Bara la Tumaini, licha ya
changamoto zinazo likabili.