2012-09-12 13:47:19

Mkutano wa Kichungaji juu ya watu watu wanaoishi barabarani wafunguliwa -Dar.


Huduma za Kichungaji barabarani : Kutembea Pamoja, ni hoja inayoongoza Mkutano wa kwanza wa Kazi za Kichungaji kwa ajili ya wanaoishi katika hali hatarishi barabarani,bila makazi ya kudumu .
Huu ni mkutano wa kibara, Afrika na Madagascar na ulifunguliwa adhuhuri Jumanne 11 Septemba 2012 huko Kurasini, katika Makao makuu ya TEC , Dar es Salaam Tanzania, kama ulivyoandaliwa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Huduma za Kichungaji kwa wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum,kwa kushirikiana na Tume ya Baraza la Maaskofu Tanzania. Mkutano huu utakao kamilika tarehe 15 Septemba , unaongozwa na aya kutoka Injili ya Lk 24:15, Yesu Mwenyewe akatokea , akatembea pamoja nao .
Mkutano huu ni mfululizo wa mikutano ya kibara, inayofanywa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum, ambayo tayari imefanyika katika zingine, huko Amerika ya Kusini mwaka 2008, Ulaya 2009, Asia na Oceania 2010. Lengo n i kuona hali halisi za watu wanaoishi katika hali hatarishi barabarani ili kubuni njia zinazofaa zaidi kutoa huduma za kichungaji kwa watu hawa, wasichana na wanawake, watu wasiokuwa na makazi ya kudumu , na pia wale wanaohusika na huduma za kusafiri barabarani mara kwa mara kama madreva wa safari ndefu nau salama wao barabarani.
Mikutano iliyofanyika katika bara zingine imetajwa kuwa ilikuwa ya kuvutia katika ngazi ya kimataifa.
Katika mkutano huu wa Dar, zaidi ya washiriki 85 kutoka mataifa 31 ya Afrika wamejiandikisha kushiriki . Kati yao wakiwa ni Maaskofu, Mapadre, Watawa na walei , wengi wakiwa ni wajumbe kutoka Tume za Mabaraza ya Maaskofu zinazohusika kazi za Kichungaji kwa wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum , pia kutoka shirika la Misaada Katoliki ngazi ya Kimataifa na Taasisi kadhaa za watawa.
Jumanne, Mkutano huu umefunguliwa majira ya mchana na kwa hotuba ya Muadhama Kardinali Polycarp Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Na pia Nunsio wa Jimbo la Papa Tanzania, Askofu Mkuu Francisco Padilla. Aidha wakati wa ufunguzi umesomwa ujumbe uliotumwa na Kardinali Tarcisio Bertone,Katibu wa Vatican kwa niaba ya Baba Mtakatifu Benedikto XV1.
Kwa kifupi Mkutano unatazama kwa kina , Waraka wa Papa ”Dhamana ya Afrika ” alioukabidhi rasmi kwa Kanisa la Afrika, Novemba 2011, wakilenga zaidi , hali halisi za wanawake , vijana na watoto wa Afrika na Madagascar, chini ya Mada kuishi pamoja. Aidha una tafakari, sura mbalimbali za kijamii na kisiasa , kwa ajili ya kutembea pamoja katika mshikamano wa kifamilia. Mengi zaidi katiak kipindi kijacho.








All the contents on this site are copyrighted ©.