2012-09-12 14:12:40

Bikira Maria, Malkia wa viumbe vyote.


Tarehe 22 Agosti, Mama Kanisa ameadhimisha Siku Kuu ya Bikira Maria , Malkia wa vimbe vyote.
Baba Mtakatifu akitoa katekesi yake kwa mahujaji na wageni Jumatano hii, aliiangalisha katika kumbukumbu hii ya kiliturujia, Mama Bikira Maria, kuitwa Malkia.
Amesema, ni Siku Kuu inayoonekana kuwa mpya , ni ya tangu kale, kama inavyoonekana katika asiliyake ya tangu mwanzo wa Kanisa , waamini kuwa na kuwa na mapenzi kwa Maria.
Siku kuu hii, ili imarishwa zaidi na Papa Pio X11, Mwaka 1954, wakati wa kuufunga mwaka wa Maria, hapo tarehe tarehe 31 May , kwa barua yake ya kichungaji juu ya Malkia wa Mbingu, iliyotolewa tarehe 11 Octoba 1954. Barua yenye kuwa na maelezo ya kina juu ya Bikira Maria, kuwa Malkia wa kila kiumbe, kutokana na ukweli kwamba, alipewa mastahili ya kupokea zawadi zote za utakatifu na hivyo kupalizwa mbinguni kiroho na kimwili.
Papa aliendelea kusema, mabadiliko yaliyofanywa baada ya Mtaguso Mkuu , katika kalenda ya liturujia , kumbukumbu hii iliwekwa kila mwaka, iwe ni kila baada ya siku nane za kuadhimisha Siku Kuu ya Maria kupalizwa Mbinguni, ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 15 Agosti, kama kielelezo cha kukazia utakatifuwa Maria kiroho na kimwili sanjari na utakatifu wa Mwanae Yesu Kristu.
Pia Papa amenukuu mafundisho ya Kanisa juu ya ”Mwanga wa Mataifa”ambamo mmeandikwa Maria alipalizwa kwa utukufu mbinguni na kufanywa kuwa Malkia wa ulimwengu, pengine kutokana ukalimifu na utukufu wa Mwanae.
Na hilo ndilo chimbuko la Siku Kuu hii ya Bikira Maria Malkia, ikionyesha mahusiano ya kipekee na Mwanae Yesu Kristu , iwe katika maisha yao ya hapa duniani, na pia katika maisha ya utukufu mbinguni.
Na kama alivyoandika Mtakatifu Efrem wa Siro, ”Ukuu wa Maria, Mama wa Bwana, Mfalme wa Wafalme, hutuonyesha, njia ya maisha, ukombozi na tumaini letu”. Na pia kama alivyoandika Mtumishi wa Mungu , Paulo V1, katika barua yake ya kichungaji juu ya Ukuu wa Bikira Maria na mahusiano yake na Kristu na kwa wote wanaomtegemea Yeye, na katika mtazamo wake na Mungu Baba , na maisha ya milele, yanamwonyesha Bikira Maria kuwa Mtakatifu sana na hazina ya zawadi zote za roho Mtakatifu.Hakuna binadamu anayemzidi Bikra Maria. Pia kama alivyoandika Mtakatifu Ildefonso , kwamba , katika kuwa rejea kwenye huduma ya ukombozi wa mwanae Yesu Kristu, Mfalme wa Wafalme” , mama huyu, aliyepewa hadhi ya kuwa Malkia wa vyote, katika huduma na Upendo.
Papa amemalizia hotuba yake , na wito unaosihi watu, kujenge mapenzi kwa mama Bikira Maria, kama jambo msingi katika maisha ya kiroho. Na pia amehimiza, katika sala, kutosahau kumgeukia Maria kwa imani. Anasema, ”Bikira Maria, daima hakosi kuingilia kati pale tunapokabiliwa na magumu kumfikia mwanae. Kwa kumtazama sana yeye , tuige imani , huruma na upendo wake mkuu katika kutimiza mpango wa upendo wa Mungu”. Maria ni Malkia wa mbingu, aliye karibu na Mungu , na pia akiwa karibu na kila mmoja wetu. Sauti yake ya unyenyevu iliyo jaa upendo wa kimama, inaita, kutushirikisha ushindi wa Mwanae Yesu Kristu, anayetawala pamoja nae katika ufalme wa milele mbinguni.








All the contents on this site are copyrighted ©.