Leo katika makala ya tafakari nasi kuhus ndoa na familia, Mheshimiwa Padre Raphael
Mwanga anachambua kuhusu dhana ya ndoa na familia katika Agano la Kale. Huu ni mfululizo
wa makala ya ndoa na familia, unaopania kuwasaidia wanandoa na familia kufahamu wajibu
wao ndani ya Jamii na Kanisa kwa ujumla. Usikose kuwashirikisha Wanajumuiya wako,
kwani kwa njia hii tunaweza kuimarisha misingi ya maisha ya ndoa na familia. Kitabu cha mwanzo
kimeweka bayana kuwa chimbuko la ndoa na familia ni Mungu mwenyewe katika uumbaji.
Jumuiya ya waisraeli kama taifa wakilishi linaongezeka lakini kama binadamu wenye
mapungufu mbalimbali yaliyoletwa na dhambi ya asili (Kitabu cha Mwanzo Sura ya 3).
Kwa sababu hiyo, sheria au taratibu za maisha zinahitajika kwa ajili ya kuondoa migongano
na pia kutunza nia ya Mungu ya uumbaji. Tufanye tafakari kidogo katika vitabu vya
kutoka, Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la torati. Taratibu za kwanza ni Amri kumiza
Mungu zilizotolewa mlimani Sinai (Kut 20:2-17, Kumb 5:6-21). ( Kut 20:14 na Kumb 5:18)
tunakutana na amri hii usizini. (Kut 20:17) usimtamani mke wa jirani yako au kumchukua
kama alivyofanya Daudi baada ya kumua Uria ( 2 Sam11-12. ). Ubikira kwa mwanamke kilikuwa
kitu cha lazima kabla ya Ndoa (Kumb 22:13-21. Umalaya au ukahaba (prostitution) Kumb.
7:3-4 Sheria ilikataza kabisa. Kuoa mtu na ndugu yake kulihesabiwa kama uchafu.Kufanya
tendo la ndoa kati ya watu wa jinsi moja au na wanyama ni tendo ambalo hakupokelewa
kwa waisraeli. Adhabu mbalimbali ziliwekwa kwa aliyekiuka taratibu ikiwa ni pamoja
na kuuawa kwa kupigwa mawe( Walawi 20:10). Je, taratibu hizi ziliwekwa kwa Waisraeli
tu au zinatuhusu sote? Ni kweli zinatuhusu sote kwani hata kwa wasioamini wanaongozwa
na dhamiri njema taratibu hizi haziko nje ya taratibu za asili zinazofumbata sheria
asilia; naamini kila mmoja wetu anaweza kuonyesha madhara ya uvunjaji wa tatatibu
hizi katika upendo wa wa ndoa, katika wajibu wa kuzaa na kulea watoto mimi katika
uzoefu wangu wa uchungaji kwa miaka tisa sasa nina mengi ya kushuhudia. Hati ya
talaka ni kweli ilikuweko katika jamii ya kiisraeli mwanamume aliweza kutoa hati ya
talaka lakini sio kwa kila jambo hasa ni katika uzinzi ambao tutauongelea zaidi katika
agano jipya Yesu anaposema Musa aliwaruhusu kutoa haki ya talaka kwa sababa ya ugumu
wa mioyo yenu lakini mambo hayakuwa hivyo tangu mwanzo, Injili ya Mtakatifu Mt. 19:3-12. Wangapi
leo wanakuja na kusema padre mimi leo nimetereza, nimeshindwa mji au ndoa imevunjika.
Ni kweli Padre anaweza kushuhudia ndoa na kuitakatifunza lakini hana madaraka ya
kusema sakramenti iliyokuwa halali imeisha nadhani watalaamu washeria za kanisa watatusaidia
sana hapa. Je hata tunapoamua kuchana kwa nguvu ni kiasi gani cha madhara tunayashuhudia
katika familia na jamii nzima? Dhana ya mke zaidi ya mmoja minatarafu Agano la
kale: Kwa ujula haikuruhusiwa kuwa na wake wengi hata kwa mfalme kama alivyofanya
Solomoni Kumb.17:17. Lakini katika mazingira maalumu iliruhusiwa kwa mfano Elkana
aliwaoa Hana na Penina 2nyakati 11:18-20, kwa sababu ya utasa hii ilimsababisa pia
Abrahamu azae na mjakazi wake Hagari: Kitabu cha Mwanzo 16. Wengi wanauliza kama
ni hivyo kwanini Kanisa halituruhusu kuoa mke au kuolewa na mume mingine endapo tumekosa
uzao? Hili lina jibu lake katika sheria ya kanisa na pia tutalijibu tutakapopata nafasi
kuelezea ndoa na sakramenti pia uzazi kwa njia ya kisayansi katika vipindi vinavyokuja.
Hivyo ninakuomba uvute subira. Kwa ujumla katika Agano la Kale watoto ni wenye
thamani kubwa (Zab 127:4-5). Ndiyo maana katika utasa ruksa ya kuoa mwingine ilitolewa
kwa ridhaa ya wana ndoa wote na ndiyo maana iliruhusiwa kumridhi ndugu yako endapo
amekufa na kumzalia ndugu yako watoto Kumb 25:5-10, na kijana aliyeoa karibuni hakuruhusiwa
kwenda vitani kabla hajazaa watoto kumb 20;7 watototo ilikuwa ni dawa ya kifo kwamba
hata wazazi wakifa wanaishi kwa njia ya watoto. Dhamani ya watoto sio katika agano
la kale tu ila ni katika kila jamii ulimwenguni, ni bahati mbaya kwamba baadhi ya
nchi zilizoendelea na zinazoendelea zimekuwa na utamaduni wa kukataa uzazi kwa hofu
ya hali mbaya ya uchumi lakini dawa ya hali mbaya ya uchumi haina maana tupunguze
watu kwani chakula kinapopungua mezani dawa sio kupunguza watu ila kuongeza chakula
tujenge mazingira ya kuzisaidia familia kubeba majukumu yake. Kutoka Studio za
Radio Vatican, ni Mimi Padre Raphael Mwanga, toka Jimbo Katoliki la Same, Mtaalam
mwanafunzi wa ndoa na familia katika taasisi ya ndoa na familia, Chuo Kikuu cha Kipapa
cha Laterano, Roma.