Sherehe ya miaka 20 ya Kanisa kuu la Mama Yetu wa Yamoussoukro
Wakatoliki wa Ivory Coast wakiadhimisha miaka 20 ya kutabarukiwa kwa Kanisa Kuu
la Mama Yetu wa Yamoussoukro, walihimizwa kujenga tumaini na nia njema kwa ajili ya
uchaguzi mkuu ujao.
Padre Stanslas Skuza , Padre Mkuu wa Kanisa hilo,
wakati wa Ibada ya Misa iliyosomwa kwa nia za kufunga sherehe hizo, aliwahimiza watu
kuutumia muda huo wa sherehe pia kutafakari kwa kina hali za taifa lao, kama maandalizi
ya uchaguzi mkuu ujao, na hasa katika kulinda na kudumisha amani nchini mwao na duniani
kote.
Na Kardinali Francis Arinze na Askofu Mkuu Ambroze Madtha, Nusio
wa Papa Ivory Coast, , wakishiriki katika sherehe hiyo, pia walihimiza waamini, kutolea
shukurani zao kwa Mungu , kwa majaliwa, upendo na huruma yake .
Kanisa la
Mama Yetu wa Yamoussuokro, lilitabarukiwa na Papa Yohane Paulo 11, Septemba 9, 1990
.